Baadhi ya watumiaji wa vyombo vya usafiri jijini
Dodoma akiwemo Athuman Salum pamoja na Khamis Maulid wamesema kupanda kwa
mafuta ya petrol na Dizeli imesababisha hali ya uchumi kuyumba .
Aidha,wameiomba
serikali kufanya mkakati wan a namna ya kushusha bidhaa hiyo muhimu.
Ikumbukwe kuwa April ,5,2022 mkurugenzi wa Petrol ,kutoka mamlaka ya udhibiti wa huduma ya nishati na maji [EWURA],Gerald Maganga alitangaza ongezeko la bei ya mafuta ya petrol kuanzia April 6,2022 ambapo bei za rejareja kwa mji wa Dodoma petrol inanunuliwa kwa Tsh.2920 kwa lita,Dar Es Salaam Tsh.2861 ,Arusha Tsh.2905,huku miji mingine mafuta ya petrol yakiuzwa Zaidi ya Tsh.3000 ikiwemo miji ya Kahama,Kigoma,Mwanza huku chanzo kikitajwa ni mgogoro wa Ukraine na Urusi.