SERIKALI YASEMA SUALA LA MAGEUZI YA SERA YA ELIMU NI KUHAKIKISHA WANAFUNZI WANAKUWA NA UWEZO WA KUJIAJIRI PINDI WANAPOHITIMU MASOMO.

0





Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kuna umuhimu wa kuongeza ubora wa  sera ya elimu ili kuhakikisha panakuwa na mageuzi ya kumwezesha mwanafunzi kujiajiri pindi anapohitimu masomo.

Prof.Mkenda amebainisha hayo  jijini Dodoma katika mkutano wa 30 wa baraza la wafanyakazi katika wizara hiyo ambapo amesema mageuzi yanahitajika Zaidi katika sekta ya elimu ili kwendana na matakwa ya mahitaji kwa wahitimu.


Kuhusu suala la kuwajengea uwezo walimu ,Prof.Mkenda amesema ni muhimu suala hilo kuzingatia ili kuweza kuandaa walimu wanaokwendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.


Akitoa neno  la shukrani  kwa niaba ya  baraza la wafanyakazi wizara ya elimu,katibu mkuu chama cha walimu Tanzania[CWT]Deus Seif amesema kuna umuhimu mkubwa wa kufanya maboresho sekta ya elimu.


Mkutano wa 30 baraza la wafanyakazi wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia umekwenda sambamba na kaulimbiu isemayo”Sensa ya Watu na Makazi ni msingi wa kichocheo cha sera bora na mipango endelevu ya elimu ,Sayansi na Teknolojia,Tushiriki kikamilifu.

MWISHO.


Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)