AFYA CALL CENTER YANG’ARA KWA KUPATA TUZO YA “DIGITAL HEALTH EXCELLENCE”

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Kituo cha kupokelea miito ya Simu na kujibu hoja mbalimbali za wananchi kuhusu masuala ya afya(199 Afya Call Center) kimepata tuzo ya Ubora katika Afya Kidijitali (Award in Digital Health Excellence) katika maonyesho ya East Africa Youth Business and Investment Expo yaliyofanyika hivi karibuni visiwani Zanzibar.


Tuzo hiyo ilikabidhiwa Agosti 10, 2025 na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Mariam Mwinyi, na kupokelewa na Dkt. Otilia Gowelle, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.


Afya Call Center imetambuliwa na kupewa tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii kupitia huduma za kidijitali zinazowawezesha wananchi kupata elimu, taarifa sahihi, ushauri wa kitaalam na uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya afya bila kujali umbali au changamoto za usafiri. Huduma hizi zimekuwa msaada mkubwa hasa wakati wa majanga ya kiafya, kampeni mbalimbali za afya, pamoja na ufuatiliaji wa magonjwa.


Tuzo hiyo pia ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Afya kutumia teknolojia za kisasa katika kuboresha upatikanaji wa huduma na taarifa za afya, sambamba na ajenda ya taifa ya mageuzi ya kidijitali ili kufikia azma ya ufikiaji wa huduma za afya kwa watu wote (Universal Health Coverage).












Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)