Na.Faustine Gimu Galafoni,Kwimba Mwanza.
Kutokana na
ukweli wa mafundisho ya Biblia
yanayotolewa na kanisa la Waadventista Wasabato,jumla ya watu 43 wamebatizwa kwa maji mengi katika
ibaada maalum ya urafiki mwema kanisa la Waadventista Wasabato Malya wilayani
Kwimba mkoani Mwanza.
Akizungumza
na mtandao huu mara baada ya kufanyika zoezi la
ubatizo kwa maji mengi ,Mchungaji wa
kanisa la Waadventista Wasabato mtaa wa Sumve Wilayani Kwimba mkoani
Mwanza Mch. Zabron Mahega Masanja
alisema hiyo ni kutokana na walimwengu kuanza kuelewa mafundisho ya ukweli wa
Biblia unaofundishwa na kanisa la Waadventista Wasabato.
“Hivyo,kanisa la Waadventista Wasbato
limekuwa ni kanisa pekee linalotoa
mafundisho ya ukweli kuhusu Biblia hivyo kutokana na ukwelli huo watu wamekuwa
wakimwamini na kumpokea Yesu Kristo baada ya kupokea mafundisho hayo ,na
kutokana na Sabato ya Urafiki mwema jumla ya watu 43 wamebatizwa kwa maji mengi
baada ya kuamini na kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yao”alifafanua Mch.Mahega
Aidha,Mch.Mahega
alitoa wito kwa watu wengine kuendelea kujitokeza na kubatizwa kwa maji mengi
kwa makanisa ya Waadventista Wasabato huku akisisitiza kwa Waadventista kuwa
nuru kwa kuwaangazia wengine ambao hawajaamini Ukuu wa Yesu Kristo.
“Wito tu kwa Waadventista kuwa nuru
kuwaangazia wengine kumpokea Yesu Kristo kwa mataifa mbalimbali””alisisitiza.
Kwa upande
wao baadhi ya watu waliobatizwa kwa maji mengi katika kanisa la Waadventista
Wasabato Malya akiwemo Evacate Jefania ,Petro Busiya Joseph ,Naomi Sambay
,Rashid Masasila pamoja na Timotheo Kasuka walisema waliamua kubatizwa
kutokana na kufuatia ukweli wa biblia
huku wakiwaasa watu wengine kumfuata Yesu Kristo.
“Kwa kweli mimi nilikuwa wa Imani
kutoka dhehebu jingine lakini baada ya kufuatilia ukweli nimeamua
kubatizwa nawasihi wengine kubatizwa kwa
maji mengi”alisisitiza
mmoja wa waliobatizwa.
Sanjari na
hayo Mch.Mahega aliwaasa Washiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa
Malya Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza kuendelea kuwa kielelezo cha kuwa na mahusiano mema ya kuishi vizuri na
jamii inayowazunguka ambapo alisema wanadamu tunategemeana katika nyanja
mbalimbali hivyo ni muhimu kuishi katika mahusiano mema.
Aidha,Mchungaji
Mahega aliainisha kanuni za kuishi
vizuri na watu kuwa ni pamoja na kudumisha upendo na kuheshimu wengine
Nao baadhi
ya wageni waliohudhuria Sabato maalum ya Urafiki mwema akiwemo diwani wa viti
maalum Julieth Mungo pamoja na
mwenyekiti wa wafanyakazi shirika la reli Tanzania [TRC]kanda ya Ziwa Akley Mirambo walielezea jinsi
walivyobarikiwa na Sabato hiyo maalum
kuwa ni pamoja na mafundisho mazuri ya Waadventista Wasabato.
“Kwa kweli
tunashukuru ukarimu mkubwa tuliofanyiwa na kanisa hili la Waadventista Wasabato
Malya kwani hii ndio dini ya kweli kujali watu”alisema Diwani Julieth.
Sabato ya
Urafiki mwema katika kanisa la Waadventista Wasabato Malya imekwenda sambamba
na utoaji wa zawadi ya vitabu vya utume
vijulikanavyo’’Jipatie amani Moyoni’’ pamoja na uwekaji mikono wakfu kwa watoto na
pikipiki ya Mchungaji mtaa wa Malya Mch.Kulwa Mbipi iliyotolewa na Jimbo
la Nyanza Kusini.
“Kwa kweli nitumie fursa hii
kuipongeza Conference ya Nyanza kusini kwa kutujali kununua usafiri wa pikipiki
hii maana eneo la Malya jiografia yake maeneo yako mbalimbali na wakati mwingine tulitembea kwa miguu au
kuazima baiskeli na waumini walinishika mkono kweli wengine waliniazimisha
pikipiki,hivyo ununuzi wa pikipiki hii yenye Zaidi ya Tsh.Milioni mbili
itasaidia sana kutembelea maeneo mengi Zaidi kupeleka injili”alisema Mch.Mbipi.