Na.Faustine Gimu Galafoni.
Imeelezwa kuwa
kuna changamoto ya baadhi ya wazazi na
walezi kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala kushiriki kutoa ujauzito kwa mabinti
zao suala ambalo ni hatari kwa afya .
Hayo yamejiri
katika ziara ya mbunge wa jimbo la Msalala wilayani Kahama Ezekiel Maige katika kijiji cha Madaho kata ya Lunguya wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga.
Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho Kazimili Pascal amesema kuwa tatizo la utoaji wa ujauzito kwa
wasichana limekuwa likisababishwa na baadhi ya wazazi.
Akijibu hoja
hiyo mbunge wa jimbo la Msalala amesema kuwa suala la utoaji mimba ni kosa la
jinai hivyo amewaomba wananchi kuwa na
ushirikiano kwa kutoa taarifa
dhidi ya watu wanaojihusisha na utoaji wa mimba.
Aidha Maige
amewaasa vijana kuepuka kuwashawishi
watoto wa kike kujihusisha na Mapenzi.