Na.Faustine Gimu ,Kahama.
Wafanya
biashara ndongondogo Maarufu kama Wamachinga
katika eneo la hospitali ya mji
wa Kahama wameandamana hadi Katika ofisi
za chama cha mapinduzi CCM kupinga agizo la mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya mji wa Kahama la kuwahamisha katika eneo hilo.
Tukio hilo
limetokea Jana majira ya saa tano asubuhi
jambo lililopelekea uongozi wa CCM
kufanya kikao cha dharura na mkuu wa wilaya ya Kahama na mkurungenzi
mtendaji wa halmashauri hiyo.
Wakizungumza
na waandishi wa habari ,baadhi ya wafanya biashara hao Saimon Nsabile na
Joshua Wiliam wamesema kuwa
wamehamishwa bila kufuata utaratibu.
Madai yao
yametupiliwa mbali na mkurugenzi
mtendaji wa halmshauri hiyo Underson Msumba ambapo amesema eneo lao
wametengewa katika eneo la CDT na hakuna machinga anayeruhusiwa kufanya
biashara eneo hilo.
Hata hivyo
wafanyabiashara hao wamepinga suala hilo wakidai kuwa eneo wanakopelekwa
haliendani na bidhaa wanazouza.
Kwa upande
wake diwani wa kata ya Kahama mjini
Hamidu Juma Kapama amesema kuwa jambo hilo ni mpango wa Mkurugenzi na halijapitishwa na baraza la madiwani.
Na.Faustine Gimu.