Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Bi.Zainabu Rajab Terack amewatakata waratibu wa TASAF Wilayani Kahama
kuwahamasisha walengwa wa TASAF kuacha
kubweteka na badala yake wajikite katika kilimo.
Hayo ameyasema katika ziara yake Mjini Kahama yenye lengo la kuhimiza wananchi kujikita katika kilimo na kuacha utegemezi.
Mkuu huyo wa mkoa
amesema kuwa msimu wa kilimo bado unaendelea ambapo amezitaka kaya masikini
kulima na walengwa wa TASAF
watakaokaidi agizo watakosa
fedha za TASAF.