Baadhi
ya viungo vya mwili ikiwemo kichwa pamoja na nguo vinavyodhaniwa kuwa ni vya Mtoto Teresia
Dickson mwenye umri wa miaka 3 mkazi wa kijiji cha Namatutu kata ya Bulungwa halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga,vimepatikana katika kijiji cha Busulwanguku kata ya Idahinha.
Akizungumza
na Baloha FM redio baba mzazi wa mtoto huyo Dickson Paul amesema kuwa mtoto huyo alipotea tangu Januari 22 mwaka huu
baada ya kwenda kucheza na watoto wenzake lakini hakulejea ndipo walipoanza
harakati za kumtafuta.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Namatutu Simon Mwendwa ameelezea juu ya kupata taarifa hizo ambapo amewataka
wanachi kuwa makini kuwalinda watoto wao.
Naye Afisa mtendaji wa kijiji
William Msoselo amezungumzia juu ya kupokea taarifa za kupotea mtoto
huyo ndipo jitihada za kumtafuta mtoto
huyo zikaanza ndipo walipoona fuvu na nguo alizokuwa amevaa.
Nao
baadhi ya wananchi mashuhuda wa tukio hilo wamesikitishwa kutokea
kwa
tukio hilo huku wakiitaka serikali kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama.
Kamanda
wa polisi mkoani Shinyanga Simon Haule ameelezea kupata taarifa
hizo na kuahidi kufuatilia ambapo uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua chanzo cha tukio hilo.