Mkuu wa mkoa wa SHINYANGA
ZAINAB TELACK amewaagiza ACACIA kuhakikisha wanatengeneza sehemu ya makazi ya
Askari ndani ya eneo la uwanja wa ndege.
Ametoa agizo hilo katika
makabidhiano ya uwanja huo wakati ukaguzi wa eneo hilo ukiendelea
ambapo amesema askari wanatakiwa kukaa sehemu nzuri ili waweze kufanya
kazi vizuri hivyo pamoja na kukabidhi wanatakiwa kutengeneza ili iwe sehemu ya
kudumu.
Kwa upande wake Meneja mkuu
wa mgodi wa Buzwagi BENADICT BUSUNZU amesema watalifanyia kazi jambo hilo ili
kuhakikisha wanaboresha na kutoa mchango kwa vitu ambavyo vitahitajika katika
uwanja huo.
Hata hivyo BUSUNZU amesema
pamoja na kukabidhi uwanja huo wataendelea kushirikiana na serikali katika
mambo mabalimbali ya kimaendeleo ili kuibua huduma ambazo zitachochea mendeleo.
Uwanja wa huo wa ndege
uliopo katika eneo la BUZWAGI Mwendakulima wilayani Kahama ulikuwa chini ya
Mgodi Wa ACACIA ambapo Januari 25 mwaka huu Umekabidhiwa rasmi mikononi mwa serikali chini
ya Naibu waziri wa Ujenzi ELIAS KWANDIKWA.