MWENYEKITI WA BUSINDI MSALALA KAHAMA ALALAMIKIWA KWA KUONGOZA KIBABE.
MBUNGE WA MSALALA EZEKIEL MAIGE
Wananchi wa kijiji cha
Busindi kata ya Bulyanhulu halimashauri ya
Msalala Wilayani Kahama, wamelamikia kitendo cha Mwenyekiti wa kijiji hicho
MUYA DOMINICK kushindwa kusoma mapato na matumizi na kuwaongoza kwa mabavu.
Hayo yameibuka katika ziara
ya Mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Maige wakati akifanya mkutano wa hadhara na wananchi
hao kijijini hapo.
Mmoja wa wananchi wa eneo
hilo FRANCISCO TUMBOWANANE akitoa kero zinazowakabili
amesema kiongozi huyo amekuwa kero kwa wananchi kwa kuwa hajawahi kusomewa mapato
na matumizi tangu mwaka 2016.
Diwani wa viti maalumu
PRISCA MSOMA ameshiriki katika mkutano huo na kusikiliza kero nyingi zikiwasilishwa
kwa Mbunge huku anasikitishwa na kinachoendelea kijijini hapo kwakuwa amesikia wananchi
wakilalamikia pia suala la kiongozi huyo kutoa nafasi za ajira zinapotokea kwa upendeleo
kwa wafuasi wa chama chake cha CHADEMA pekee.
Mwenyekiti huyo anayetupiwa
lawama akijibu hoja zilizoibuliwa na wananchi amekiri kutoa upendeleo wa ajira zinapojitokeza
na kuwapa wanachama wa cha CHADEMA
kwakuwa ni wafuasi wa chama chake huku akisema amekuwa akishindwa kusoma mapato
na matumizi kwakuwa nyaraka zimepotea.
Kufuatia sakata hilo Mbunge
wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige amemwagiza diwani wa Kata hiyo John Kiganga kulifuatilia.
Ziara ya Mbunge huyo inaendelea
tena kesho katika maeneo mengine ya jimbo hilo ikiwemo Kijiji cha Sungamile.