Ikiwa kesho
shule mbalimbali hapa nchini zinatarajia
kuanza masomo baada ya likizo baadhi ya
vifaa vya shule mjini Kahama vimepanda bei kutokana na uhitaji kuwa mkubwa kwa
wanafunzi ikilinganishwa na hapo nyuma.
Hayo yamesemwa
leo na baadhi ya wateja wa mahitaji ya vifaa vya shule ambao ni wazazi wa
wanafunzi walipokuwa katika
manunuzi soko la uwanja wa taifa eneo la Majengo mjini Kahama.
Wazazi hao
wamesema kuwa wafanyabiashara wamepandisha bei
kwa bidhaa za shule baada ya kuona kuna wateja wengi huku wakiwaasa
watoto wao kusoma kwa bidii katika kipindi hiki kigumu kwani elimu ni ufunguo
wa maisha.
Kwa upande wao
baadhi ya wafanyabiashara wa vifaa vya shule ikiwemo viatu na nguo wamesema
kuwa biashara imekuwa nzuri kwao na sababu ya kupandisha bei ni kutokana na
uhitaji mkubwa.
Naye mmoja wa
wanafunzi ameahidi wazazi kusoma kwa bidii
kwani wazazi wake wamekuwa wasaidizi wakubwa katika masuala yake ya
shule.
Shule
mbalimbali za msingi na sekondari hapa nchini zinatarajia kufunguliwa kesho
Januari 8 ,tayari kwa kuanza muhula mpya wa Masomo 2018 na wanafunzi kupanda
ngazi mbalimbali za madarasa na vidato.