Jamii wilayani
Kahama mkoani Shinyanga imeaswa kudumisha mila na desturi za kitanzania kwa kupinga mauaji ya vikongwe
na watu wenye ualbino.
Hayo yamesemwa
na mtemi wa Sungusungu wilayani Kahama mkoani Shinyanga Machimu Mwanandalo katika kilele cha kongamano la Mwanandalo la
kudumisha mila na desturi lililofanyika
kata ya Mwakata Halmashauri ya Msalala.
Mwanandalo
amesema kuwa ni vyema jamii ikawa na uelewa juu ya vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikiwadhalilisha waganga havina budi
kupingwa vikali na serikali.
Nao baadhi ya
wanachi waliohudhuria akiwemo diwani wa kata ya Mwasala Mkoani Tabora
wamezungumzia juu ya kongamano hilo.
Kitikiti Masai ni
mwakili wa Sadick Kisenga ambapo
ameelezea juu ya zawadi hiyo ambayo amekabidhiwa mwenyekiti wa Sungusungu Wilaya ya Kahama Machimu
Mwanandalo..
Kongamano la mila na desturi la Mwanandalo 2018
limeenda sambamba na upokeaji wa zawadi ya trekta moja aina ya S.H lenye thamani ya Sh.milioni 20 na gari Landcruiser
moja lenye thamani ya shilingi milioni 40 yote yametolewa na Mfanyabiashara maarufu kutoka mkoani Morogoro
Sadick Kisenga baada ya kufurahishwa na kongamano hilo