Katika kuelekea kuadhimisha kilele cha kutimiza miaka 41 ya chama cha mapinduzi CCM tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977,chama cha mapinduzi kata ya Nyasubi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kimetembelea kituo cha kulelea watoto wanaoishi mazingira hatarishi Cha MUVUMA Nyasubi na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.
Akizungumza
katika eneo la kituo hicho,Katibu wa CCM kata ya Nyasubi Mlawa Nyili amesema kuwa Lengo la kufika kituoni hapo ni kuwafariji
watoto na kujionea changamoto zao huku akitaja baadhi ya msaada wa vitu
walivyotoa.
Mwenyekiti
wa CCM kata ya Nyasubi Bathelomeyo
Kayoka ameitaka jamii Wilayani
Kahama kuwa na tabia ya kusaidia watoto
waishio katika mazingira hatarishi na kuacha tabia ya unyanyapaa kwani nao ni
binadamu kama watu wengine.
Walezi wa
kituo hicho Anatulia Petro na Eliya Mpenda wameomba jamii nyingine
iwe na moyo kama huo huku wakikiomba
chama cha mapinduzi CCM kuendelea kutoa misaada .
Kwa upande
wao watoto wanaolelewa katika kituo cha MUVUMA wamekipongeza chama cha
mapinduzi CCM kwa kutoa msaada huo.