Mkuu wa wilaya
ya Kahama mkoani Shinyanga Fadhil Nkurlu amewapa pole wananchi wa
kahama kwa tatizo la maji lililo kuwepo kwa zaidi ya wiki moja
Mkuu huyo wa
wilaya amesema kuwa tatizo hilo limekuwa likijitokeza kutokana na mamlaka ya
maji ya mjini shinyanga kashuwasa kwa kukatiwa huduma ya umeme kutokana na deni
wanalodaiwa na shirika la umeme na hivyo kuathiri upatikanaji wa maji.
Aidha amesema
kutokana na hali hiyo leo ameketi na bodi ya maji ya kuwasa ili kuweza kutafuta
ufumbuzi wa kudumu ili tatizo hilo lisijirudie tena kwani limekuwa
likisababisha watu kukosa maji safi na salama.
Katika hatua
nyingine Nkurlu amewapongeza wazazi
waliojitokeza kuwaandikisha elimu ya msingi,pamoja na kuongezeka kwa idadi ya
wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza.
Amesema
kumekuwa na jitihada binafsi anazozifanya baada ya kukutana na kufanya
mazungumzo na muwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa nchini na kumuomba kutatua
changamoto mbali mbali ikiwemo katika sekta ya elimu.