REA YAFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA NISHATI SAFI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mha. Advera Mwijage, amesema taasisi hiyo inaendelea kuwa na  mapinduzi makubwa katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia na nishati jadidifu

Ambapo mapinduzi hayo  yameendelea kuonyesha ufanisi mkubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo, baada ya kuanza rasmi utekelezaji wa mradi kabambe wa ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta maeneo ya vijijini.

Mha.Mwijage amesema hayo wakati akizungumza na wadau waliotembelea banda la REA katika Maonesho ya Nane Nane jijini Dodoma ambapo amesema mkakati huo unalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za nishati na kuchochea kasi ya ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa maeneo husika.

 
"Lengo letu kuu ni kuhakikisha wananchi wote wanapata nishati salama, nafuu na endelevu ili kuboresha maisha yao, kuongeza fursa za biashara na uwekezaji, pamoja na kulinda mazingira," amesema Mha. Mwijage.


Mha. Mwijage amewakaribisha wananchi na wadau wote kutembelea banda la REA kwenye maonesho hayo ili kujionea mafanikio ya miradi mbalimbali na kujifunza fursa lukuki zinazopatikana kupitia sekta ya nishati vijijini.



Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)