FAIBA MLANGONI MAENDELEO YA UCHUMI KIDIJITAL NCHINI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 




Na Avelina Musa - Dodoma.

Kadri matumizi ya teknolojia yanavyoendelea kuongezeka, upatikanaji wa intaneti ya uhakika unakuwa msingi wa maendeleo ambapo Faiba Mlangoni kupitia TTCL ni mfano Bora  wa huduma zinazolenga kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa intaneti na kuifanya iwe karibu zaidi na wananchi.

Faiba Mlangoni inalenga kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa urahisi bila usumbufu wa taratibu ndefu na  kumfanya mteja aanze kutumia intaneti kwa haraka na kwa urahisi.


Akizungumza katika maonesho ya nane nane Jijini Dodoma Meneja wa Biashara kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania Mkoa wa Dodoma Bi.Leyla pongwe amesema huduma ya Faiba Mlangoni imeboreshwa ili kuwapatia wananchi intaneti ya uhakika kwa matumizi ya kilimo na  biashara kidijitali, burudani na huduma nyingine zinazohitaji kasi kubwa ya intaneti. 


Bi.Lyela amesema TTCL inaendelea kusogeza huduma zake karibu na wananchi kwa lengo la kuunga mkono maendeleo ya uchumi wa kidijitali nchini.


"Wananchi wanaotembelea banda la TTCL wanapata fursa ya kupata elimu kuhusu namna ya kujiunga na huduma ya Faiba Mlangoni, kujisajili papo hapo pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa shirika kuhusu suluhisho mbalimbali za mawasiliano na TEHAMA."Amesema.



Amesema huduma hiyo ni Suluhisho kwa familia na Biashara ambapo inasaidia kuhakikisha kila mwanafamilia anaweza kutumia intaneti kwa mahitaji yake bila usumbufu na kwa wafanyabiashara, intaneti ya uhakika huchangia mawasiliano bora na wateja, matumizi ya mifumo ya malipo na uendeshaji wa biashara kwa ufanisi zaidi.





Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)