MHE. KUNTI MAJALA AFANYA ZIARA YA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI JIMBO LA CHEMBA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 




Mbunge wa Jimbo la chemba Mhe. Kunti Majala amefanya mkutano wa hadhara wenye lengo la  kusikiliza kero za Wananchi katika kata ya Gwandi na kutoa Ufafanuzi wa Changamoto zilizowasilishwa ya miundombinu ya barabara,mawasiliano pamoja na  Migogoro ya ardhi.



Mhe. Kunti amefanya mikutano hiyo   katika vijiji 3 na kitongoji 1 vinavyounda kata ya Gwandi ambapo  imefanyika katika Kijiji Cha Muungano huku akitoa vifaa vya michezo jezi na mpira.

Aidha katika Kijiji Cha Rofati, Mhe.Kunti ametoa vifaa vya michezo jezi na mpira
 na katika kijiji Cha gwandi, alitoa vifaa vya michezo jezi na mpira pamoja na kitongoji Cha Toroma.


Hata hivyo wananchi wa kata ya Gwandi wamemshukuru na kumpongeza Mhe. Kunti Majala kwa kutatua kero zao pamoja na kumkabidhi  zawadi mbali mbali.




 

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)