PICHA:DKT. HINGORA KATIKA MKUTANO WA PEN PLUS AFRIKA,ASISITIZA UMUHIMU WA LISHE.

MUUNGANO   MEDIA
0





Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Rahma Hingora akiwa katika picha za matukio mbalimbali kwenye Mkutano wa kimataifa wa PEN-Plus Africa Conference uliofanyika katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC).


 Katika Mkutano huo Dkt. Hingora amesema  lishe bora ni msingi wa kinga dhidi ya magonjwa sugu.

Amesema katika sehemu ya elimu ya afya kwa umma (health promotion), Wizara imewaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo mamalishe na babalishe ili kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa chakula salama na chenye afya kwa wananchi.

Ameeleza kuwa lengo ni kuhakikisha chakula kinachopikwa na kuuzwa kwa wananchi kinazingatia viwango vya lishe bora, ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya chumvi nyingi, mafuta na viambato visivyo na afya.


Amesema kupitia ushirikiano huo, jamii inapaswa kuhamasishwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia kama mboga za majani, maziwa, karanga na vyakula vingine vyenye virutubisho muhimu ili kupunguza hatari ya magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari na magonjwa ya moyo.

Aidha, ameongeza kuwa juhudi hizo zinalenga kuimarisha afya kuanzia ngazi ya kaya, hospitali na maeneo ya biashara, kwa lengo la kujenga jamii yenye afya bora na kupunguza mzigo wa magonjwa yasiyoambukiza nchini.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)