WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAOMBA KUIDHINISHIWA BIL.137.8 KWA MWAKA 2026/27

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Na Avelina Musa - DODOMA.


WIZARA ya Viwanda na Biashara yaiomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Shilingi bilioni 137.8 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya viwanda na biashara nchini.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga wakati akiwasilisha bajeti hiyo Bungeni leo Mei 22, 2026 jijini Dodoma ambapo amesema Shilingi bilioni 33.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha zote za maendeleo zikitokana na vyanzo vya ndani vya Serikali.


Mhe.Kapinga amesema bajeti hiyo inalenga kuendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kuongeza uzalishaji wa viwanda vya ndani, kukuza biashara na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi.



Aidha amesema kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 104.1 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ambapo Shilingi bilioni 78.0 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na Shilingi bilioni 26.0 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo ya uendeshaji.


Amesema katika Mwaka 2026/2027 wizara imepanga kuimarisha ushirikiano wa biashara baina ya Nchi na Nchi, Kikanda na Kimataifa kwa ajili ya kuongeza ushindani wa sekta ya biashara kwa kufuata kanuni na mtangamano wa biashara.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)