SEKTA YA VIWANDA YACHOCHEA UPATIKANAJI WA AJIRA 39,250 NCHINI.

MUUNGANO   MEDIA
0


 

Na Avelina Musa - DODOMA.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Judithi Kapinga amesema Tanzania imeendelea kuandika historia mpya katika sekta ya viwanda na biashara huku Serikali ikiendeleza juhudi za kujenga uchumi wa kisasa unaotegemea uzalishaji wa ndani, kuongeza thamani ya malighafi na kukuza ajira kwa wananchi. 


Waziri Kapinga amesema hayo leo Mei 22, 2026 bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, mafanikio makubwa yameendelea kushuhudiwa ambapo viwanda vipya vikubwa na vya kati 25 vimejengwa na kuanza uzalishaji katika maeneo mbalimbali nchini. 


 Amesema ukuaji huo wa sekta ya viwanda umechochea upatikanaji wa ajira 39,250, zikiwemo ajira za moja kwa moja 7,635 na zisizo za moja kwa moja 31,615. Serikali inaeleza kuwa mafanikio hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayolenga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)