Na Avelina Musa - Dodoma.
Imeelezwa kuwa Juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha uchumi wa buluu na sekta ya uvuvi zimezaa matunda ya Mapato kutokana na shughuli za uvuvi kuongezeka kutoka shilingi bilioni 4.4 mwaka 2020 hadi bilioni 8.2 mwaka 2025.
Mkoa wa Mwanza umeendelea kunufaika kwa kiasi kikubwa na mageuzi katika sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki, hasa kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa katika uzalishaji na usindikaji wa mazao ya samaki.
Hayo yameelezwa leo Julai 16 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita,ambapo amesema idadi ya vizimba vya kufugia samaki (fish cages) imeongezeka kutoka 1,664 mwaka 2020 hadi 2,715 mwaka 2025, sawa na ongezeko la vizimba 1,051.
Mhe.Mtanda amesema Mkoa utaendelea kuhamasisha uwekezaji, utafiti na matumizi ya teknolojia ili kuhakikisha wananchi wa Mwanza, wakiwemo wavuvi wadogo na wafanyabiashara wa dagaa, wananufaika ipasavyo na rasilimali za Ziwa ambapo alisema katika kipindi cha mwaka 2024 zaidi ya tani 43,657.6 za minofu ya samaki zilichakatwa huku tani 81,812 zikisafirishwa nje ya nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
"Kilo za mabondo zilizosafirishwa kwenda soko la nje ya Nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwanza zimeongezeka kutoka kilo 431,721 mwaka 2020 hadi kilo 495,448 mwaka 2024 sawa na ongezeko la kilo 63,727 na Idadi ya mabwawa ya ufugaji wa Samaki imeongezeka kutoka 286 mwaka 2020 hadi mabwawa 531 mwaka 2025 sawa na ongezeko la mabwawa 245. Kiasi cha mapato yaliyotokana na shughuli za uvuvi kimeongezeka kutoka Shilingi 4,416,172,821.59 mwaka 2020 hadi Shilingi 8,233,724,351.33 mwaka 2025 sawa na ongezeko la Shilingi 3,817,551,529.74."Amesema mhe.Mtanda.
Kwa upande wa Sekta ya Maji Mhe.Mtanda amesema MWAUWASA kuanzia Julai 2020 hadi Mei 2025, imekamilisha jumla ya miradi 80 yenye thamani ya Shilingi 100,338,450,084.06 ambayo imepelekea hali ya upatikanaji wa maji vijijini kuimarika kwa kiwango kikubwa kutoka 57% 2021 hadi 77% mwaka 2025.
"Wilaya ya Kwimba imetekeleza miradi 29 ya maji katika vijiji mbalimbali pamoja na uchimbaji wa visima 22, Kwa gharama Shilingi22,046,262,574.43, Wilaya ya Magu ilipokea Shilingi. 13,479,505,945.97 kwa utekelezaji wa miradi ya maji, uchimbaji wa visima 19 katika vijiji 5,Wilaya ya Misungwi ilipokea jumla ya Shilingi. 21,210,784,588, ambapo miradi ya thamani ya Shilingi. 7,122,836,106.08 imekamilika na ile ya Shilingi. 14,087,948,482.50 inaendelea kutekelezwa na Wilaya ya Sengerema imetekeleza miradi 27 ya maji yenye thamani ya Shilingi. 40,464,136,499.74 pamoja na uchimbaji wa visima 13."Amesema Mhe.Mtanda.
Kwa upande wa Biashara na Uwekezaji,Mkoa wa Mwanza Idadi ya Viwanda Vikubwa imeongezeka kutoka 46 mwaka 2020 hadi viwanda 50 mwaka 2025 sawa na ongezeko la viwanda 4. Idadi ya viwanda vya kati imeongezeka kutoka 109 mwaka 2020 hadi viwanda 116 mwaka 2025 sawa na ongezeko la viwanda 7.
"Idadi ya viwanda vya kati imeongezeka kutoka 109 mwaka 2020 hadi viwanda 116 mwaka 2025 sawa na ongezeko la viwanda 7. Idadi ya viwanda vidogo na vidogo sana imeongezeka kutoka viwanda 1,776 mwaka 2020 hadi viwanda 2,322 kwa Mwaka 2025 sawa na ongezeko la viwanda 546"alisema.
Amesema Sekta ya kilimo Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 640,205.3 (37.59%) 2020/21 hadi kufikia tani 1,025,784.08 (60.23%) mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la Tani 385,578 (22.64%).
Aidha Mtanda amesema Katika kuboresha maslahi ya wakulima, mfumo wa kununua mazao kupitia vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) vimeongezeka kutoka vyama 164 mwaka 2018 hadi vyama 257 mwaka 2025 pamoja na upatikanaji wa mbolea ya Ruzuku umeongezeka kutoka tani 249.4 Mwaka 2020 hadi 3,611.25 mwaka 2025 sawa na ongezeko la tani 3,361.8.
"Ujenzi na ukarabati wa miradi ya umwagiliaji 2 ya Sengerema Katunguru na Mahiga kwimba kwa gharama ya Shilingi. 54,473,623,973.41 unaendelea Upatikanaji wa viuatilifu umeongezeka kutoka chupa 324,821 Mwaka 2020 hadi chupa 832499 Mwaka 2025."Alisema Mtanda.
Mkoa wa Mwanza ulipokea jumla ya Shilingi Trilioni 5.6 kipindi cha mwezi Novemba, 2020 hadi Aprili, 2025 kwa ajili ya maendeleo ya sekta mbalimbali .
.jpg)

