BRELA YAWAITA WAKAZI WA DODOMA KUFIKA KATIKA MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Na Avelina Musa - Dodoma.


Wakala wa Usajili wa biashara na Leseni(BRELA) yawaita wakazi wa Dodoma na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kufika katika Banda lao ili kupata huduma na Elimu  ya usajili wa biashara  na leseni.



Hayo yamesemwa na Afisa Leseni Mwandamizi Koyan Abubakari kutoka Brela wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma  yanayoendelea katika viwanja vya Chinangal Park Jijini Dodoma.



Abubakar amesema lengo la Brela kushiriki katika wiki ya Utumishi wa Umma ni kusogeza huduma na kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua majukumu ya Brela na kusajili biashara pamoja na kupewa leseni za biashara zao.





"Huduma tunazozitoa  ni kusajili leseni ya  biashara,Kusajili majina ya biashara,Kusajili  viwanda vidogo,Usajili wa alama za biashara ambapo kusajili jina la biashara ni Tsh.20,000 ili mfanyabiashara aweze kufanya majukumu yake bila bugdha."Amesema Abubakar.



Kwa upande wake mmoja wa wananchi aliyepata huduma katika Banda la Brela Bi  Nzurika Zavala ambaye ni mjasiriamali ameishukuru Brela kwa kumpatia huduma nzuri ambapo anasema amepata ushirikiano tofauti na ulivyotarajia.





"Nimepata ushirikiano mzuri na tayari nimepewa cheti changu mwanzo nilidhani nitasumbuliwa kuwa Rudi baada ya siku kadhaa" amesema Nzurika.






Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)