BALOZI CHENGULA ASEMA MITAMBO MIPYA ILIYOZINDULIWA INAENDA KUWAKOMBOA WACHIMBAJI WADOGO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Na Avelina Musa -Dodoma


 
BALOZI wa Amani Duniani ambaye pia ni Mwakilishi wa Wachimbaji wadogo Mkoani Geita Bw.Methew Chengula amesema mitambo mipya ya uchorongaji madini iliyozinduliwa Leo inaenda kuwakomboa wachimbaji wadogo  na  kuiongezea mapato serikali.

 

Bw.Chengula amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma mara baada ya uzinduzi wa mitambo hiyo ambapo amesema mitambo hiyo inaenda kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kwa Wizara ya Madini la kuwaangalia kwa jicho la tatu wachimbaji wadogo.



Mapema leo June 24.2025 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  amezindua mitambo mipya ya uchorongaji wa madini kwa wachimbaji wadogo wadogo ambayo imetolewa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).



“Mitambo hii inaenda kutatua changamoto kubwa lakini nimekuwa nikijihusisha sana na mambo ya teknolojia,Kuna wachimbaji tunaendelea kuwapa elimu hii inakuja kuweka utafiti wa asilimia 98 ni kitu kizuri kwani inaenda kuongeza tija na serikali inazidi kunawiri kwa sababu itaongeza mapato,”amesema Chengula




Chengula ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya mahusiano kati ya wachimbaji na jamii kutoka Shirikisho la Wachimbaji madini Tanzania( FEMATA) amesema  ameendelea kutoa elimu kuhakikisha amani inaendelea kuwepo kwa wachimbaji nchini.



“Ndio maana utaona sehemu nyingi katika migogoro na kuwemo kwa sababu ya kutafuta amani kwani amani inatakiwa kusemwa kila mahali,”amesema Chengula.



Aidha,Kwa upande wake  Msanii Maarufu wa Dansi nchini,Komandoo Hamza Kalala amesema ataendelea kusema mazuri yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita huku akidai ikifika Octoba watapiga kura ya tiki kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika nafasi ya urais.



“Nina umri wa miaka 54  chochote kilichofanywa na Nchi hii na mimi nitakuwa mmoja wao nina  wimbo wa wembe ni ule ule,Serikali yetu imefanya mambo makubwa ambayo tunatakiwa kuyasemea,”amesema Komandoo.





Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)