DKT.GWAJIMA ASEMA SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA JAMII INAPATA TAARIFA SAHIHI KUHUSU ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 




Na Avelina Musa - Dodoma.


Katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya kupinga dawa za kulevya Duniani,Waziri wa Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dkt Doroth Gwajima amesema Serikali  imejidhatiti kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kuhusu hatari na athari  za matumizi ya dawa za kulevya. 



Ambapo serikali imeweka  mikakati mitatu  katika kukabiliana na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo kuwakamata wafanyabiashara wanaofanya biashara hiyo.



Mhe,Gwajima ametaja mikakati hiyo  Jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la vijana liloandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA).



Waziri Gwajima amesema mkakati mojawapo  ni kutoa elimu sahihi katika suala la  tiba pamoja na kuimarisha ushirikiano  na jamii ili kuleta tija katika ujenzii wa taifa.



Mhe.Gwajima amesema tatizo la dawa za kulevya linahatarisha afya na mustakabali wa vijana na vinaweka hatarini  maendeleo  pamoja na jamii na taifa kwa ujumla.



“Adhari zake ni pana kama nilivyosema kama vile mfumo wa afya uliozidiwa  ,kuongezeka uhalifu na nguvukazi isiyoweza kuchangia ipasavyo uchumi wetu  hivyo elimu sahihi ni nyenzo muhimu katika vita dhidi ya matumizi ya dawaza kulevya,”amesema Waziri Gwajima



“Niwatake vijana na wasomi kuwa ni muhimu kuelewa uzito wa tatizo la dawa za kulevya na kulitatua nakutambua jukumu lenu katika kulitatua hata hivyo wanapaswa kulinda mazingira yanayowazunguka”



“Ninawahimiza kuwa mabalozi wazuri wa mtindo wa maisha bila dawa za kulevya, andikeni maandiko ya kampeni na uhamasishaji tumieni ubunifu kueneza ujumbe unaoeleza kuwa kuna nguvu katika kufanya maamuzi mazuri kwa kuwasaidia wale wanaokabiliwa na uraibu wa madawa ya kulevya,”alisema Waziri Gwajima



Kwa upande wake,Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) John Lyimo amewataka vijana kutokuwa na imani potofu kuwa ukitumia dawa za kulevya unaelewa katika masomo  na kujua vitu vingi.

“Wengi  wanaojiingiza katika matumizi wanaondoka katika masomo na  future yao inaishia hapo kutokana na matumizi tu dawa hizo,”amesema Kamishna Jenerali

Kamishna Lyimo amesema  wanaotumia dawa wengi ni vijana wadogo wenye umri wa kuanzia miaka 12 ambapo amesema  Serikali imejenga sehemu ya kutoa tiba pamoja sober kwa ajili ya kupata matibabu kwa vijana hao.




Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)