WATUMISHI TDB WATAKIWA KUZINGATIA MISINGI YA UWAJIBIKAJI NA WELEDI KATIKA MAJUKUMU YAO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 





Na Avelina Musa - Dodoma.


Watumishi wa Bodi ya maziwa Tanzania (TDB) wametakiwa kuwa weledi katika majukumu yao Kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji na uaminifu katika majukumu  na kutunza Siri za wateja na Serikali.


Kauli hiyo imetolewa  na Kaimu katibu Mkuu Wizara ya mifugo na Uvuvi Dkt.Charles Mhina Jijini Dodoma wakati  akizungumza Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.Riziki Shemdoe wakati akizungumza na watumishi wa Bodi ya maziwa katika kikao kazi Cha kuboresha utendaji  kazi kwa watumishi hao.

Dkt.Mhina amesema kila mtumishi anatakiwa kutekeleza majukumu yake kutokana na mpango mkakati wa taasisi na kujua kanuni za utumishi na misingi ya utawala Bora.

"Tunapaswa kuwa waaminifu  kwa mteja pamoja na kuwajibika ipasavyo ili kuwaridhisha wateja au wadau tunaowahudumia, Kila mtumishi anapaswa kujiuliza je anafanya kazi yake vizuri na ni Kwa namna gani umetoa huduma bora kwa wateja wako na watumishi wenzio".

Aidha,Ameipongeza Bodi ya Maziwa Tanzania  kwa kuandaa kikao kazi hicho kwani itawajengea uzoefu mkubwa na kufanya kazi Kwa weledi unaotakiwa na kutoa huduma Kwa wakati,kama huduma inapaswa kutolewa ndani ya siku 3 basi iwe ivyo ili Kujenga uaminifu kwa mteja.

"Niwasihi msitoe  Siri za taasisi kama wewe sio msemaji wa taasisi sio vizuri kutoa taarifa ambazo sio sahihi maana saivi watu wanapenda kusambaza na kupotosha taarifa ambazo sio sahihi na zinaleta taharuki kwenye jamii jambo ambalo sio sawaa na unakuwa mtumishi ambaye sio mwadilifu"amesema Dkt.Mhina.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya maziwa Tanzania Prof.George Msalya amesema wana mpango wa Kuanzisha Baa za maziwa ili ziweze kusaidia watu ambao hawako huru na lengo ni kuhamasisha unywaji wa maziwa nchini kwa  kuanzisha baar za maziwa.



Prof. Msalya amesema bar hizo za maziwa zitakuwa maeneo maalumu ambapo wananchi wataweza kufurahia aina mbalimbali za maziwa na bidhaa zake kama vile mtindi, siagi, maziwa ya ladha tofauti.

"Uanzishaji wa baa hizi ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuongeza matumizi ya maziwa kwa kila mtu, ambayo bado ni ya chini ukilinganisha na viwango vinavyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO),"Amesema Prof.Msalya.

Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)