Na Avelina Musa - Dodoma.
licha ya ongezeko la watu katika Jiji la Dodoma.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso Jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji safi nzuguni awamu ya pili uliofanyika katika ofisi za mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Dodoma DUWASA.
Ambapo mamlaka hiyo imeingia mkataba na mkandarasi Bahaji Construction work wenye thamani ya shilingi Bilioni 5.6 unaotegemewa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi 15.
Mhe. Aweso amesema wizara ya Maji haitakuwa kikwazo katika kuhakikisha wakazi wa Dodoma wanapata Maji safi na salama.
Aidha Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 15 ambapo zaidi ya wananchi laki moja na Elfu ishirini na tatu watanufaika na mradi huo.
"Mradi huu utaleta unafuu wa upatikanaji wa maji katika maeneo ya Nkuhungu,Miganga,Mkonze,Chidachi na Makulu Ostabey"Amesema Mhandisi.
Naye Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde amesema zoezi la utiaji saini ni sehemu ya utatuzi wa changamoto ya maji katika jiji la Dodoma kutokana na uhitaji wa huduma hiyo kwa baadhi ya maeneo yenye Mgao.
Naye Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde amesema zoezi la utiaji saini ni sehemu ya utatuzi wa changamoto ya maji katika jiji la Dodoma kutokana na uhitaji wa huduma hiyo kwa baadhi ya maeneo yenye Mgao.
Hata hivyo ikumbukwa kuwa Eneo la Nzuguni mpaka sasa lina Visima Tisa vilivyokamilika ambavyo vina uwezo wa kuzalisha maji wastani wa lita milioni Ishirini kwa siku ambapo hadi kukamilika kwa awamu ya pili ya mradi huu itasaidia kuongeza hali ya uzalishaji maji kutoka lita milioni 81 hadi 90 kwa siku sawa na ongezeko la asiliami 30 kutoka kwenye chanzo hicho.