ELIMU YA AFYA KUTOLEWA MAONESHO YA WIKI YA WANAWAKE ARUSHA.

MUUNGANO   MEDIA
0



Na.Elimu ya Afya kwa Umma.


Katika Maonesho ya Wiki ya Wanawake ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Arusha.


Wizara ya Afya haijaachwa nyuma katika kushiriki maonesho hayo ambapo katika Banda la Wizara ya Afya Huduma na elimu ya Afya inatolewa kuhusu:


Elimu ya Afya juu ya umuhimu wa kutumia vyakula vilivyorutubishwa.

kupima uwiano wa urefu kwa uzito (BMI)

Lishe kwa Rika Barehe.

 


Huduma zingine zinazotolewa ni pamoja na uchunguzi wa awali wa Saratani ya Mlango wa Kizazi, vipimo kuhusu Magonjwa ya moyo na vipimo vingine vingi.


Kumbuka, Elimu ya Afya na Huduma ya vipimo vinatolewa bila malipo,mahali ni uwanja wa Michezo wa Kumbukumbu ya Shekhe Amri Abeid ambapo yameanza tarehe 1,Machi,2025 hadi siku ya kilele tarehe 8,Machi, 2025.


Kaulimbiu ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu ni “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji” ambayo imetokana na Kaulimbiu ya Kimataifa ‘’For All Women and Girls. Equality. Rights. Empowerment’’. Lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kukuza Usawa, Haki na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana na kwa kuzingatia kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ili, wajiamini, wajiandae na wajitokeze kugombea nafasi za uongozi.


MWISHO.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)