Na Avelina Musa - Dodoma.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), imeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuboresha huduma za majisafi na uondoaji wa majitaka kwa wakazi wa Jiji la Arusha.
Kupitia juhudi hizi, AUWSA imeongeza upatikanaji wa majisafi, kupanua mtandao wa majitaka, na kupunguza upotevu wa maji, sambamba na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) Mhandisi Justine Rujomba wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akielezea mafanikio na mwelekeo wa Mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita leo Machi 14,2025.
Mhandisi Rujomba amesema uboreshaji wa huduma ya Majitaka wamefanikiwa kupanua mtandao wa kukusanya Majitaka kutoka asilimia 8.03 kwa mwaka 2020/21 hadi asilimia 39.5 mwaka 2024/25 pamoja na kununua magari manne ya kunyonya Majitaka yenye uwezo wa kubeba lita 5,000 na 10,000.
"Mafanikio Katika Upatikanaji wa MajisSafiKatika mwaka wa fedha 2024/25, upatikanaji wa huduma za ya majisafi umeongezeka kwa kiwango kikubwa. AUWSA imeendelea kupanua mtandao wa usambazaji majisafi ili kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wakazi wa mijini wanapata huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 95 ifikapo 2025. Aidha kwa eneo la Jiji la Arusha kwa kupitia Mradi mkubwa, AUWSA imefanikisha upatikanaji wa majisafi kwa asilimia 99.2".
" Uboreshaji wa Huduma ya Majitaka AUWSA imepanua mtandao wa kukusanya majitaka kutoka asilimia 8.03 (2020/21) hadi asilimia 39.5 (40) mwaka 2024/25. Aidha, ili kuwahudumia wananchi ambao hawajafikiwa na mtandao wa majitaka, Mamlaka AUWSA imeongeza idadiimenunua ya magari manne ya kunyonya majitaka (Sewer BowsersCesspit Emptier Trucks) hadi kufikia matano, yenye uwezo wa kubeba lita 5,000 na 10,000. Majitaka yanayokusanywa kutoka kwa wateja zaidi ya 10,930 yanatibiwa katika mabwawa ya kutibu majitaka yaliyopo Terrat (Themi Holding Ground) ambapo majitaka hayo yaliyotibiwa yanawanufaisha wananchi walipo kusini mwa mabwawa hayo kwa kutumia maji hayo yaliyotibiwa kwa ajili ya shughuli za kiuchumi ikiwemohususani kilimo cha umwagiliaji".
Aidha amesema kuwa mbali na kuongeza upatikanaji wa majisafi na kupanua mtandao wa majitaka pia wameweka jitihada za katika kupunguza upotevu wa maji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.
Mhandisi Rujomba amesema katika Jiji la Arusha upatikanaji wa huduma ya maji umeongezeka kutoka saa 16 (2020/21) hadi saa 22 mwaka 2024/25 na kuongezeka kwa idadi ya wateja waliounganishwa na huduma za maji kutoka 71,183 (Juni 2021) hadi 134,000 kwa sasa.
Hata hivyo amesema kupitia ufadhili wa Serikali ya Tanzania Pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), AUWSA imekamilisha mradi mkubwa wa maji kwa lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa majisafi na kuboresha huduma ya uondoaji wa majitaka katika jiji la Arusha ili kuboresha afya na hali ya maisha ya wakazi wa Jiji kwa ujumla wake ambapo Mradi huu umegharimu Shilingi za Kitanzania Bilioni 520 na Kazi zilizofanyika ni pamoja na:Uchimbaji wa visima virefu,Ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka,Ujenzi wa mtambo wa kutibu majisafi katika chanzo cha mto - Midawe,Ujenzi Upanuzi wa mtandao wa majitaka nje pembezoni mwa Mjiya jiji,Ujenzi wa vyoo vya mfano katika shule na masoko,Ujenzi wa Ofisi za Kanda na Ofisi Kuu kwa lengo la kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi pamoja naUpanuzi wa mtandao wa majisafi.
Mwisho.