Waipongeza M-mama (115).
199 nayo yapewa Kongole.
Na. Elimu ya Afya kwa Umma.
Kikundi cha Uimbaji cha *Wanawake na Samia* wanaoishi katika kambi ya watu wenye Changamoto ya Ukoma cha *Wasamaria* kata ya Hombolo Mkoani Dodoma wamempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha Sekta ya Afya.
Wakizungumza katika Makazi hayo ya *Wasamaria* baadhi ya Wanakikundi hao cha Wanawake na Samia wamesema upatikanaji wa umeme vijijini(REA) umerahisisha kuimarika kwa huduma za afya pamoja kupatikana kwa maji ambayo hutumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo usafi katika kujikinga na Magonjwa ya mlipuko.
Mary Sambay ni mmoja wa Kikundi hicho cha sanaa kutoka Makazi ya Wasamaria anasimulia kuwa hapo awali walikuwa wanatumia Kibatali na chemli katika vituo vya kutolea huduma za Afya lakini kwa sasa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) imeondoa changamoto hiyo.
"Nyakati za usiku tulikuwa tunatumia kibatali na chemli tuponaenda kupata huduma za afya lakini kwa sasa umeme umerahisisha hivyo tunamshukuru sana Rais kwa kufanya juhudi kubwa pia M-mama 115 inasaidia sana kwa usafiri wa dharura kwa Mama na Mtoto mchanga" amesema.
Moloni Timotheo amesema upatikanaji wa umeme vijijini umerahisisha kuwepo kwa mashine za kupumulia Watoto wachanga.
"Upatikanaji wa umeme vijiiji unasaidia sana sisi akina mama mfano ile mitambo hospitalini ya kupumulia watoto Wachanga na pia imeturahisisha upatikanaji wa maji safi na salama ya uhakika"amesema.
MWISHO.