MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA(TMDA) YAELEZA MKAKATI WAKE KATIKA KUHAKIKISHA WATANZANIA WANAKUWA SALAMA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Avelina Musa- Dodoma.


Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba ( TMDA) imewasihi watanzania wanapopata changamoto yoyote kama wametumia bidhaa za dawa na vifaa tiba wasisite kurudi Katika maeneo ambayo walipata huduma ya afya.


Hayo yameelezwa na Meneja wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba Kanda ya kati Sonia Mkubwa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la maonesho ya nanenane Nzuguni jijini Dodoma huku akiwataka wananchi kutembelea Banda hilo kwa ajili ya kutambua huduma zinazotolewa kwenye Banda hilo.


Sonia amesema Katika kuhakikisha bidhaa na vifaa hivyo vinakuwa Bora , salama na fanisi ni lazima wahakikishe na kusajili bidhaa kabla hazijaingia sokoni.


Aidha amesema pamoja na majukumu hayo lakini pia wanapima na kusajili dawa na majengo ili yaendane na Sheria ili huduma zinazotoka pale ziwe Bora na zenye stahiki.


"Sisi pia tunaangalia usalama wa dawa na vifaa tiba lengo likiwa ni kujali afya ya watanzania wenzetu" alisema Sonia.


Ikumbukwe kuwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ni Taasisi iliyopo chini ya wizara ya afya ambayo inajukumu kuu la kuhakikisha kwamba inalinda afya ya jamii.


Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)