TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA(THBUB) YALAANI KITENDO CHA BINTI KUFANYIWA UKATILI.

MUUNGANO   MEDIA
0


Na Avelina Musa - Dodoma.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imelaani kitendo cha video inayosambaa katika mitandao ya kijamii inayoonyesha vijana watano wakimbaka na kumlawiti binti ambapo imesema kitendo hicho sio cha kiungwana na hakikubaliki popote.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 7,2024 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye banda la tume hiyo lililopo katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzunguni.

"Sisi kama Tume tunaona binti huyo alifanyiwa unyanyasaji na amenyimwa haki yake za ubinadamu wake, utu wake amedharirishwa katika utu wake na vilevile ni kitendo ambacho hakikubariki kwasababu kinaonekana kiliandaliwa nani bahati mbaya sana kwamba inaonekana kiliandaliwa na mtu ambaye alikuwa anafahamu kinachoendelea", amesema.

Mwaimu amesema wanaamini ofisi ya mashtaka itaweza kuwafungulia watu hao mashtaka ili sheria iweze kuchukua mkondo wake na wakikutwa na hatia waweze kupatiwa adhabu kali.

Ikumbukwe kuwa Agosti 4, mwaka huu zilisambaa video katika mitandao ya kijamii zikiwaonyesha vijana watano wakimbaka na kumlawiti binti huyo, huku wakimtuhumu kwa kile kilichosikika katika video hiyo kuwa ametembea na mume wa mtu.

Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)