Na Avelina Musa - Dodoma
Bodi ya Bima ya Amana(DIB)lenye jukumu muhimu katika usimamizi na udhibiti wa sekta ya bima nchini imesema itaendelea kudhibiti , kusimamia na Kufuatilia kampuni zote za bima kuhakikisha zinazingatia sheria na kanuni ili kuweka viwango vya maadili na kuimarisha uwazi katika utendaji wa kampuni za bima.
Hayo yameelezewa Leo Agosti 7.2024 na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)na Mwenyekiti Wa bodi ya wakurugenzi Wa Bodi ya Bima ya Amana Emmanuel Jutuba kwenye maonesho ya wakulima nane nane yanayoendelea Nzuguni Jijini Dodoma .
Jutuba amesema majukumu ya bodi hiyo ni kukagua na kutoa leseni kwa kampuni za bima ili kuhakikisha zinafaa kuendesha shughuli za bima ambapo ametaja majukumu mengine kuwa ni pamoja na kutathmini Malalamiko kwa kupokea na kuyatatua kutoka kwa wateja kuhusu huduma za bima.
Aidha amewataka wananchi kutembelea banda la Bodi ya bima ya amana kujifunza zaidi ambapo wanapaswa kuelewa kuwa wanaendeleza na kuboresha mazingira ya biashara ya bima kwa ajili ya kukuza ukuaji wa sekta ili kuhakikisha sekta ya bima inafanya kazi kwa ufanisi na kwa faida ya wateja.
Ameeleza ukubwa wa mfuko huo kuwa hadi kufikia June 30,2023 Mfuko wa bima ya amana ulikuwa na shilingi Trilioni 1.04 ambazo zimetokana na mchango wa Serikali wa shilingi Bilioni 1.05 ambazo zilitolewa wakati wa kuanzisha mfuko mwaka 1994 na kufafanua kuwa hadi kufikia June 30,2024 mfuko ulikuwa na wanachama 44.
Mbali na hayo ameeleza muundo wa Bodi hiyo kuwa upimo chini ya Mamlaka ya Bodi ya wakurugenzi ambayo ina jukumu la kuunda Sera na kuhakikisha utawala bora.
Ikumbukwe kuwa DIB ni Taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya benki na Taasisi za fedha ya mwaka 1991 ambapo ilianza kufanya kazi zake mwaka 1994 chini ya usimamizi wa BOT.
Mwisho.