Katika utekelezaji wa Kampeni ya Mtu ni Afya, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda, leo Agosti 10, 2024 ameongoza mamia ya watu kwenye matembezi maalumu ya TEMEKE WALKATHON yaliyoandaliwa na Hospitali ya Rufaa ya Temeke iliyopo Dar es Salaam
Matembezi ya za Kilomita 8 kwa 5 yalianzia viwanja vya Mwembe yanga kuzunguka na kuishia mwembe yanga jijini Dar es salaam Shabaha yake ikiwa ni kuchangia vifaa kwa watoto waliozaliwa kabla ya miezi tisa katika hospitali ya rufaa ya Temeke.
Ni muhimu kila mmoja kufanya mazoezi katika kuimarisha Kinga ya Mwili.
#UsibakiNyuma #MtuNiAfya
Fanya kweli Usibaki nyuma,Mtu ni Afya.
Kwa taarifa,Elimu na Ushauri zaidi Piga Simu 199