Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu leo tarehe 10, Agosti,2024 ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa jengo la Huduma Jumuishi ikiwemo Huduma za Uchapaji (HPS Printing Press),Studio lililopo katika eneo la Njedengwa, Jijini Dodoma.
Dkt. Jingu ameambatana na Viongozi mbalimbali wa Wizara akiwemo Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizara ya Afya.
Ikumbukwe kuwa jengo hilo litakapokamilika litawezesha shughuli mbalimbali za Wizara kufanyika hapo ikiwemo huduma za uchapaji wa vitabu, vipeperushi, miongozo, Kalenda, kadi, mafaili, mabango, Tshirt na vielelezo mbalimbali vya afya, Kituo cha Afya Call Center(199), Studio kwa ajili ya matangazo na vipindi vya Uelimishaji na uhamasishaji kuhusu masuala mbalimbali ya Afya pamoja na ukumbi wa mikutano.
Jengo hilo jumuishi la Elimu ya Afya kwa Umma ambalo ujenzi wake ulianza mwaka 2022 linatarajia kukamilika hivi karibuni na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa.
MWISHO.