SSP MARIA KWAY: ELIMU IENDE SAMBAMBA NA MSAADA WA MAHITAJI MUHIMU

MUUNGANO   MEDIA
0



Mkuu wa Polisi Wilaya ya Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Maria Kway ametembelea na kutoa msaada wa vitu na fedha kiasi cha shilingi 130,000/= kwa familia ya Bi. Elinara Anyingisye mwenye ulemavu wa Ngozi (Albino)  nyumbani kwake Kijiji cha Majengo kata ya Mkwajuni Wilaya ya Songwe


SSP Kway, aliambatana na baadhi ya askari Polisi katika tukio hilo la kutoa msaada huo kwa familia hiyo ili kuongeza   upendo kwa jamii.

Vilevile SSP Kway alitoa wito kwa jamii kuendelea kujitoa kuwasaidia wenye uhitaji mbalimbali na kutowaacha kuzagaa mtaani na kujikuta wakifanyiwa ukatili au kujiingiza kwenye matendo ya kihalifu.




SSP Kway amewahakikishia usalama familia hiyo kufuatia tabia ya baadhi ya watu wenye imani za kishirikina kuvamia, kujeruhi na kuwauwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa matumizi ya imani za kishirikina ambayo sio sawa na wote wenye tabia kama hiyo hawataukwepa mkono wa sheria.

Kwa upande wake Bi. Elinara Anyingisye  kwa niaba ya familia yake amelishukuru Jeshi la Polisi kwa msaada huo walioupata na ameahadi kuendelea kutoa ushilikiano kwa Jeshi la Polisi Pindi aonapo viashiria vya kutaka kufanyiwa ukatili ili aendele kuishi salama.

Mahitaji ambayo amekabidhiwa tarehe 24 Julai mwaka 2024 ni Kofia 01, Dera 01, Viatu pair 04, Sabuni ya Unga, Sabuni ya miche 04, Sweta 03, Begi za Shule 03, Mpunga debe 06, Daftari dozen 03, kalamu za wino na risasi Pedi 2 dazeni, Mafuta ya kupaka carton 1, Miswaki, Sketi, kaptula na shati 3 za Shule Solar 01, Brashi, Soksi na nguo za ndani za watoto vyote vikiwa na thamani ya shilingi 368,000/= ambapo fedha za matumizi na vifaa imegharimu shilingi  490,000/=
Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)