VIONGOZI WOTE TABORA WAAGIZWA KUTEKELEZA MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII.
Author -
MUUNGANO MEDIA
Jumanne, Juni 11, 2024
0
Mhe. Paul Matiko Chacha Mkuu
wa Mkoa wa Tabora.
.
Na. Elimu ya Afya kwa Umma.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora,Mhe. Paul Matiko Chacha amewaelekeza viongozi wote
ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuhakikisha kuwa wanatekeleza mpango
Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kwa mujibu wa Miongozo ya
Serikali.
Mhe. Chacha ametoa maelekezo hayo Juni 10,2024 wakati
amefungua Kikao cha kujadili Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu
wa Afya Ngazi ya Jamii Mkoani Tabora.
Aidha, ametoa shukrani kwa
Wadau wote wanaoendelea kushirikiana na Serikali ya awamu ya Sita chini
ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika kuboresha huduma za afya nchini.
Halikadhalika,
amesisitiza kuwa kuwa katika Mkoa wa Tabora Serikali inaendekea kufanya
mambo mengi katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa
mpango huu utaokuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Tabora huku
akiipongeza Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuweka Mkoa wa
Tabora miongoni mwa mikoa ya kipaumbele.
Naye Katibu Tawala wa
Mkoa huo Dkt. John Mboya amewahimiza Viongozi na wajumbe wote kuepuka
vitendo vyote kinyume na mwongozo katika ngazi zote.Dkt. John Mboya,Katibu Tawala wa
Mkoa huo.
Wajumbe wa kikao hiki ni Viongozi mablimbali wa Mkoa na Halmashauri zote nane (8) wakiweno Wakuu wa Wikaya na Wakurugenzi.