WAZIRI UMMY ATOA WITO KWA JAMII KUWA NA UMUHIMU WA MIUNDOMBINU RAFIKI NA JUMUISHI KWA HEDHI SALAMA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa wito kuendelea kuhamasisha utoaji wa elimu , ujenzi wa Miundombinu rafiki na jumuishi kwa ajili ya hedhi salama, uwekezaji wa uzalishaji wa vifaa vya hedhi salama na watengenezaji kuweka “package” ya mwanafunzi ili kuwapa urahisi na unafuu katika upatikanaji wa taulo za za kike.


Wito huo umetolewa Jijini Dodoma leo Tarehe 22,Mei, 2024 na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa kwa Wanahabari kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Hedhi Salama na Uzinduzi wa Maadhimisho hayo

"Wito wa Serikali ni kuendelea kuhamasisha utoaji elimu, ujenzi wa miundombinu rafiki na jumuishi kwa ajili ya hedhi salama, uwekezaji wa uzalishaji wa vifaa vya hedhi salama na watengenezaji kuweka “package” ya mwanafunzi ili kuwapa urahisi na unafuu katika upatikanaji wa bidhaa hizi"amesema Mhe.Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema Hedhi isiyo salama ina athari za kiafya ikiwemo kupata magonjwa kama UTI na magonjwa mengine ya njia ya Uzazi, pia huongeza hatari ya kupata ugumba kutokana na utumiaji vifaa vya hedhi visivyo salama.

Mbali na athari za kiafya pia Waziri Ummy amesema , inaathari kwenye shughuli za maendeleo ya mwanamke katika nyanja zote ikiwemo elimu, ushiriki kwenye shughuli za kijamii na uchumi.

Halikadhalika, Waziri Ummy amefafanua maana ya Hedhi Salama ni pamoja na kuhakikisha msichana na mawanamke anapata elimu sahihi ya hedhi na huduma katika mazingira salama yenye miundombinu ya vyoo vyenye usiri.

"Tunaposema hedhi salama maana yake ni kwamba msichana na mwanamke anapata elimu sahihi ya hedhi salama, anapata huduma katika mazingira salama yenye miundombinu ya vyoo vyenye usiri, maji safi na salama, vifaa salama vya kujisitiri na utupaji salama wa vifaa vya hedhi vilivyotumika", Waziri Ummy"amesema Waziri Ummy.






Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)