Na.Pendo Mangala, Dodoma
Wadau Pamoja na Taasisi mbalimbali za Manumuzi wamekutana Jijini Dodoma kujadili mchakato wa kuandaa kanuni za rufaa za ununuzi wa Umma za Mwaka 2024 ambapo kanuni hizo zitatoa wigo mpana wa kuwasilisha malalamiko ambapo mabadiliko hayo yatawapa wazabuni fursa ya kushindana kwa haki na uwazi katika zabuni mbalimbali.
Akizungumza katika kikao kazi hicho cha kutoa maoni kilichofanyika Mei 22,2024 Jijini Dodoma, na Kamishna wa Sera za Ununuzi wa Umma,Dk.Fredrick Mwakibinga Wizara ya fedha ambaye amemuwakilisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ,Jenifa Omolo katika kikao kazi hicho.
Dk.Mwakibinga amebainisha kuwa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) ipo katika mchakato wa kuandaa Kanuni za Rufaa za Ununuzi wa Umma za mwaka 2024 ambapo pamoja na mambo mengine, kanuni hizo zitatoa wigo mpana wa kuwasilisha malalamiko iliwa ni Pamoja na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa watumishi na Wazabuni.
“Ikumbukwe kuwa shughuli zote za ununuzi wa Umma zinafanyika kwa njia Kieletroniki kupitia mfumo wa NeST na kwa kuwa moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko yanayotokana na michakato ya Ununuzi wa Umma nayo imekamilika katika mfumo wa NeST na inatarajiwa kuanza kutumika mwezi Julai 2024,”’Amesema
Sanjari na hayo,Kamishina huyo ,ametoa rai kwa aTaasisi za u nunuzi, zijitqhidi kutoa maoni yatakayowasaidia kuepukana na malamiko yasiyo na ulazima .
"Nina uhakika kupitia kikao hiki tutapata maoni na michango mizuri ambayo itaiwezesha Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma kupata Kanuni za Rufaa za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2024 zinazoendana na wakati na zitakazoiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha katika ununuzi wa Umma"
"Napenda niwapongeze PPAA Pamoja na Wizara ya Fedha na Ofisi ya Wanasheria Mkuu wa Serikali kwa kusimamia zoezi la uandaaji wa Kanuni hizi zitakazo iwezesha Serikali kutumia rasilimali zake kwa wakati, uwazi na haki"Amesema
Katika hatua nyingine amesema anatambua kuwa washiriki wa Kikao kazi cha leo ili kuiwezesha Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kupokea maoni yatakayowezesha uandaaji wa Kanuni za Rufaa za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2024. ni muhimu kuwasilisha kwa uwazi maoni yatakayowezesha uandaaji wa Rasimu ya Kanuni za Rufaa za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2024 .
"Umuhimu huo unachagizwa na mabadiliko ambayo yanaendelea kufanyika katika sekta ya Ununuzi wa Umma nchini. Ambapo hivi karibuni, tumeshuhudia kutungwa Sheria ya Ununuzi wa Umma Na 10 ya mwaka 2023,sheria hii mpya ya Ununuzi wa Umma imeboresha masuala mbalimbali ikiwepo kupunguzwa kwa muda wa kushughulikia malalamiko na rufaa zinazotokana na michakato ya Ununuzi wa Umma,mfano, muda wa siku saba (7) za kazi kwa ajili ya kusubiri malalamiko ya wazabuni (cool off period) kabla ya kutoa tuzo umepunguzwa na kuwa siku tano (5) za kazi. Muda huo hautajumuisha njia za ununuzi ambazo hazihitaji ushindani kama vile single source, minor value procurement na shopping"
"Muda wa Afisa Masuuli kushughulikia malalamiko ya zabuni umepunguzwa kutoka siku saba (7) za kazi hadi siku tano (5) za kazi pale ambapo hataunda jopo. Endapo Afisa Masuuli ataunda jopo la mapitio ya malalamiko basi atakuwa na siku saba (7) za kazi na atatakiwa kuwajulisha washiriki wote wa zabuni juu ya uundwaji wa jopo hilo, sambamba na hilo muda wa PPAA kushughulikia malalamiko au rufaa umepunguzwa kutoka siku arobaini na tano (45) hadi siku arobaini (40)"Amesisitiza
"Ni imani yangu kuwa kupitia kikao kazi hiki maoni ya wataalamu wetu mliokusanyika hapa leo yatasaidia kupata kanuni bora zinazoendana na mazingira ya sasa"
Kwa upande wao baadhi ya washiriki akiwemo Liipu Rweyemamu Wakala wa huduma za Ununuzi Serikalini amesema kuwepo kwa utoaji wa maoni hayo itasaidia kuleta manufaa kwani sheria ya Sasa ina mabadiliko mengi ikiwemo kutumia muda mfupi katika kushughulikia malalamiko.
Mwisho