Suala hili linadhihirisha kwamba mtandao wa Intanenti ni muhimu katika suala zima la mawasiliano katika ulimwengu huu wa Sayansi na Teknolojia.

Kukosekana kwa huduma za mtandao,upatikanaji wa intaneti unazuiliwa au kuzuiliwa kwa muda fulani, ni suala linalozidi kuwa na athari kubwa katika jamii zetu za kidijitali katika baadhi ya nchi za afrika.
Kutokana na hili baadhi ya Vijana na wanawake wametoa ushauri kwa wafanyamaamuzi na wanaharakati kuhakikiksha wanasimamia suala la mtandao kuhakikisha Mawasiliano ya mtandao yanakuwa huru wakati wote hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kudai kuwa ni haki yao ya msingi.

Wameeleza kuwa wakati uliopo sasa ni wa Kidijitali kutokana na Dunia kuwa Kijiji ambapo mawasiliano ya mtandao yanatumika kuendesha shughuli mbalimbali za maendeleo na kama Vijana kwao inakuwa ni tatizo kutokana na kukosa Fursa za kazi na biashara kupitia mitandao.
Sanjari na hilo wameomba Elimu zaidi iendeleeebkutolewa kwa jamii kuhusu athari za kuzimwa kwa mtandao kwa manufaa ya Taifa.
Tumeshuhudia kuwepo kwa taarifa mbalimbali kupitia Mitandao ya kijamii ikiwemo Fursa za Ajira Pamoja na sponsa za masomo hivyo ni muhimu suala la mtandao likapewa kipaumbele kama zilivyo huduma nyingine za kijamii kama Maji,Afya nakadhalika.

Kutokana na kutangazwa kwa nafasi za Ajira na Jeshi la Polisi Nchini Mei10 Mwaka 2024 taarifa zimesambaa kutokana na kuwepo kwa Mitandao wa Intaneti ambao vijana wameonekana kuchangamkia fursa wengine kuwepo katika sehemu za kutolea huduma za mitandao ya Internt (Internet Cafe) lakini kukosa huduma .
Kukosekana kwa huduma ya mtandao wa intaneti imetokqna na hitilafu ya kiteknolojia na kusababisha
.jpeg)
Kituo hichi kimewashujudia vijana hao na kuzungumza nao juu ya umuhimu wa internet ambapo wamesema suala la matumizi ya internet ni muhimu kwa tija Zote kwani Ni Nyanja ya kiuchumi.
“Naomba haya tu atakuwa kutuma kwa njia ya mtandao lakini kuwepo kwa tatizo lakukosekana kwa mtandao imesababisha kushindwa kutuma maombi tovuti haifunguki hivyo ni tatizo kwetu nakuomba Serikali kuongeza muda wa maombi,””Wamesem
Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara kwanjia ya mtandao wamesema kutokana na hitilifu ya Kukosekana kwa huduma ya mtandao wa intaneti umewasababishia hasara kutokana na huduma hiyo kukosekana.
Mnamo mei 12 Mwaka 2024 Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Ulifika taarifa kuwepo kwa tatizo la mtandao nchini na kuahidi kuishughulikia changamoto hiyo.
MWISHO