Na Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma
Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kwa kushirikiana na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) inaendesha Mafunzo ya afya ya uzazi kwa vijana kwa watumishi wa Kituo cha Huduma ya simu cha Wizara ya Afya (Afya Call Centre-199) Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Kituo hicho, Beatrice Titho amesema lengo la mafunzo hayo ya siku 5 yanayoendelea kuanzia Mei 20-25, 2024 ni kuwajengea uwezo watumishi hao kwenye eneo la Afya ya Uzazi kwa Vijana na kuelezea matarajio yake kuwa baada ya mafunzo hayo watumishi hao wataweza kujibu maswali na hoja mbalimbali ambazo zilikuwa zikiibuliwa na vijana kuhusu masuala ya afya ya uzazi.
Hali kadhalika wananchi hususan vijana wataweza kupatiwa taarifa sahihi zaidi kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi.
Miongoni mwa mada zinazojadiliwa ni pamoja Hali Halisi ya Afya ya Uzazi kwa Vijana, Umuhimu wa kuwepo Huduma za Afya ya Uzazi kwa Vijana, sera na Mwongozo wa Taifa kuhusu afya ya Uzazi na Mtoto, Mabadiliko ya Kijana Balehe, Mambo yanayoathiri afya ya uzazi kwa vijana, Uzazi wa Mpango, Magonjwa ya Ngono, Ukatili wa Kijinsia na Saratani ya Mlango wa Kizazi.
Hongera Sana Kwa mafunzo haya.
WATUMISHI AFYA CALL CENTER (199) WAPEWA MAFUNZO YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA
Alhamisi, Mei 23, 2024
0
Tags