WAHITIMU KIDATO CHA SITA WAITWA KUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT.

MUUNGANO   MEDIA
0




 Na .Aveline Musa, Dodoma


JESHI la kujenga Taifa (JKT )limetoa wito kwa Vijana waliohitimu Kidato cha sita kwa Mwaka 2024 kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria ili kujengewa uzalendo na stadi za maisha.



Hayo yameelezwa  Mei 24,2024  Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma na Brigedia Jenerali Hassan Mabena  Mkuu wa  tawi la utawala wa JKT,wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu wito huo wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria Mwaka 2024 .


Ametaja kambi ambazo vijana hao wamepangiwa kuwa ni JKT Rwamkoma-Mara,JKT Msange-Tabora,JKT Ruvu-Pwani,JKT Mpwapwa,Makutupora JKT-Dodoma,JKT Mafinga-Iringa,JKT Mlale-Ruvuma,JKT mgambo na JKT Maramba-Tanga.


Aidha,amezitaja Kambi nyingine ni JKT Makuyuni-Arusha,JKT Bulombora,JKT Kanembwa na JKT Mtabila-Kigoma,JKT Itaka-Songwe,JKT Luwa na JKT Milundikwa-Rukwa,JKT Nachingwea-Lindi,JKT Kibiti-Pwani na Oljoro JKT-Arusha.


Hata hivyo  Jeshi hilo limeonya baadhi ya watu wasio waadilifu kuacha vitendo vya kitapeli kwani mafunzo hayo yanatolewa bure huku Jeshi hilo likibainisha kuwa Vijana watatakiwa kuripoti wakiwa na Vifaa mbalimbali ikiwemo Shuka za kulalia.


“Tunawataka vijana kuripoti wakiwa na vifaa ambavyo watavipata na orodha kamili ya majina ya Vijana hao na Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo ya makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz,”amesema Brigedia Jenerali Mabena.


Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)