WAZIRI JAFO AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA NISHATI SAFI

MUUNGANO   MEDIA
0





 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.

Dkt. Selemeni Jafo amesema takwimu zinaonesha watu milioni nne

barani Afrika wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na matumzii ya

nishati chafu ikiwemo ya kuni na mkaa.

Hivyo, amesema ajenda ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya

kuanzisha kampeni ya kuhamasisha nishati safi Afrika inapaswa kuungwa

mkono na watu wote.

Amesema kuwa matumizi ya kuni na mkaa nchini yanasababisha hekta

takriban 46,242 kupotea kila mwaka kwa kukatwa kwa ajili ya kupata

kuni na mkaa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1,500 yakiwa

na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha tarehe 27 Aprili, 2024

wakiwemo wajasiriamali, Dk. Jafo amesema hatua hiyo inaunga mkono

juhudi za Rais Samia katika kampeni ya kuhamasisha nishati safi.

“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amekuwa na dhamira njema na ndio

maana amekuja na kampeni ya nishati safi ya kupikia.Haya ni mapenzi

yake na kwasababu tunafahamu nishati chafu inamadhara makubwa

katika mazingira.

“Kwanza watu wanalazimika kutegemea kuni na mkaa kwa hiyo kuna

uharibifu wa mazingira. Takwimu zinaonesha kila mwaka hekta 4,6242

zinapotea kwasababu ya kuni na mkaa,”amesema Dkt. Jafo.

Pia amesema takwimu zinaonesha kuwa wakinamama na wasichana kwa

asilimia kubwa wanatumia wastani wa saa 20 kwa wiki kwa ajili ya

kutafuta kuni na mkaa au wakati mwingine ni kinyesi cha wanyama.

“Leo hii ukiona nchi imejipanga katika nishati safi ya kupia ni jambo la

msingi lenye kutia matumani.Watafiti wanatuambia kitendo cha kutumia

nishati safi ya kupikia kwa akina mama wajazito kunasaidia kurekebisha

presha ya mama mjazito,”amesema.

Ameongeza pia nishati safi inasaidia mama mjazito kupata mtoto

mwenye uzito unaokubalika anapozaliwa , hivyo kuna faida nyingi

kutumia nishati safi ya kupikia.


“Nina fahamu mpaka leo hii Oryx wameshatoa mitungi ya gesi 32,000

kwa ajili ya jamii na wameshatumia Sh.bilioni 2.7 lakini bado

wameendelea kuendelea na kampeni hiyo kwa kutoa mitungi kwa jamii.

Ameongeza kuwa Oryx wamekuwa mfano mzuri kuifikia jamii huku

akifafanua tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwa taasisi zinazoanzia

watu 100 kufunga mfumo wa kutumia nishati safi ya kupikia na tayari

taasisia na mashirika ya umma yameanza kutumia nishati hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema

katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia kuhamasisha nishati safi

ya kupikia wameona ni vema kuendelea kuyagusa makundi mbalimbali

katika jimbo hilo.

Amesema kuwa kabla ya kugawa mitungi hiyo 1,500 ya Oryx kwa wana

Arusha Mjini, tayari ameshagawa pia mitungi 1400 kwa wajasiriamali

huku akisisitiza wataendelea na kuyafikia makundi yote yakiwemo ya

watoto wanaolelewa vituo vya ya watoto yatima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Bw.

Benoite Araman amesema madhara yanayotokana na kutumia kuni na

mkaa ani makubwa na kuwa wananchi 33,000 wanapoteza maisha kila

mwaka kwa kuvuta moshi na chembe chembe zinazotokana na mkaa na

kuni, hivyo kupikia gesi itatatua jambo hili.

Amesema kupika kwa kutumia gesi huchochea kutokukatwa kwa miti

kwa ajili ya kuni na mkaa hivyo, husaidia kulinda mazingira na wakati

huo huwafanya wanawake wasitumie muda mwingi kutafuta kuni na

msituni hatua itakayosaidia maandalizi ya chakula kwa wakati.

"Oryx Gas Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutekeleza

maono ya Rais kuhusu upatikanaji wa nishati. Namshukuru Mbunge wa

Arusha Mjini Gambo na Serikali ya Tanzania kwa kutuunga mkono katika

mipango yetu ya nishati safi kwa kuhakikisha matumizi ya gesi ya Oryx

hapa Arusha na Tanzania kwa ujumla,". Amesema Bw. Araman

Wakitoa shukrani zao Wajasiriamali Bi. Asha Mtumwa na Bw. Karim

Abdallah wakieleza kuwa hatua hiyo ya kukabidhiwa mitungi ya gesi

inakwenda kuwaondolea adha waliyokuwa wakiipata kwa muda mrefu.

Wamesisitiza kuwa inaenda kuondoa athari ambazo zimekuwa

zikijitokeza kwa matumizi ya kuni na mkaa ambapo inaathari kuanzia

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)