Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameielekeza timu ya usimamizi wa huduma za afya mkoa kuimariisha usimamizi wa utoaji chanjo ya surua na rubela ili kuepuka taarifa za upotoshaji.
Amebainisha hayo Leo Jumatano Februari 14,2024 wakati akizungumza na wanahabari mkoani hapa.
Amesema chanjo zitakazotolewa katika kampeni hiyo ya kitaifa ni zile zitolewazo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
"Natoa rai kwa wananchi wote kuepuka taarifa za upotoshaji kuhusiana na huduma za chanjo,"amesema Mrindoko.
"Mtoto asiyepata chanjo ni hatari kwa afya yake na jamii inayomzunguka,anaweza kuambukizwa au kuambukiza wengine kwakukosa Kinga,"
Hata hivyo watoto kuanzia umri wa miezi 9 hadi miaka mitano watapata chanjo hiyo huku mkoa wa Katavi ukitarajia kuchanja watoto 171,965.
Manispaa watoto watakaopata chanjo hiyo ni 28,702, Tanganyika 57,656, Mlele 10,017, Mpimbwe 34,083 na Nsimbo 41,453 utekelezaji wake utaanza February 15,2024
