Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na
waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska
Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo tarehe 10 Desemba
2023. Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amewaasa watanzania
kutumia vema mitandao ya kijamii. Amesema matumizi yasiofaa ya mitandao ya
kijamii yamekuwa yakiumiza watu wengi hivyo yampasa kila mmoja kutumia vema
pamoja na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.
Makamu
wa Rais amewashukuru waumini hao kwa kuendelea kumuombea ili aweze kutekeleza
vema majukumu yake.