Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha huduma ya Chakula ni ya Uhakika kwa wahanga katika kijiji cha Katesh. Baadhi ya wahanga wameshukuru sana jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Rais Samia kwa kuwafanya wajisikie kuwa na amani muda wote licha ya maafa yaliyowakumba.





