WANAOTOROSHA MADINI KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Uploading: 687750 of 2123487 bytes uploaded.




Na. Gideon Gregory, Dodoma.
Waziri wa Madini,Anthony Mavunde amesema kuwa hatoangalia sura ya mtu wala cheo kwa mtu ambaye atabainika anatorosha Madini nje ya nchi kutokana na wimbi hilo kuongezeka.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Septemba 11,2023Jijini Dodoma wakati wa kikao Cha pamoja kati ya wachinbaji wadogo waliopo chini ya shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini Tanzania (FEMATA) ambapo amebainisha mikakat. itakayo saidia kukuza uchumi wa wachimbaji na sekta hiyo.

“Kuhusu utoroshaji naomba tushirikiane nitasimamia sheria, sitosita kuwachukulia hatua wale wote wanatorosha madini, sitaangalia sura ya mtu, nitahakikisha nasimamia kwa dhati na naamini kwa kushirikiana tutafanikisha kumaliza kabisa hilo tatizo, mimi na wenzangu tutakuwa wakali sana katika hili, milango yangu itakuwa wazi tushirikiane,” amesema Mavunde. 
'image.png' failed to upload. TransportError: There was an error during the transport or processing of this request. Error code = 7, Path = /_/BloggerUi/data/batchexecute : Unknown HTTP error in underlying XHR (HTTP Status: 0) (XHR Error Code: 6) (XHR Error Message: ' [0]')


Akizungumzia juu ya kuongeza taarifa za utafiti wa jiolojia Mhe.Mavunde amesema kuwa moja ya vipaumbele vyake katika sekta ya madini ni kuijengea uwezo Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili iweze kufanya utafiti wa kina kwa ndege yaani (Air Born Geophysical Survey) utakaotoa taarifa zitaonesha utajiri wa madini yaliyopo nchini kwa kiwango kikubwa tofauti na sasa ambapo ni asilimia 16 tu ya eneo lote nchi nzima limefanyiwa utafiti wa kina.
Uploading: 1578432 of 1578432 bytes uploaded.



“Ndugu zangu tukipiga picha ya miamba yote nchi nzima, tutapata taarifa sahihi ya kijiolojia ili wachimbaji wasifanye kazi zao kwa kubahatisha , uchimbaji ni Sayansi sio bahati wala uchawi, mchimbaji mwenye taarifa ya utafiiti wa kijiolojia atafanikiwa zaidi kupitia Sekta hii ya Madini” amesema Mavunde.

Amesema utafiti huo utatoa taarifa kwa kina na utaleta tija na mapinduzi makubwa katika sekta nyingine akitolea mfano sekta ya kilimo hasa katika utafiti wa udongo,mbolea na sekta ya maji katika uchimbaji visima.
Uploading: 589500 of 2051481 bytes uploaded.


Sambamba na hayo amezungumzia kuhusu Madini ya Kimkakati ambapo amesema kuwa kwa mwelekeo wa dunia ya sasa madini hayo yanakwenda kuwa na soko kubwa na kwamba Tanzania haitajiweka kando, kwa kuwa mtizamo wa dunia ni kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kutumia nishati safi.

“Madini ya Kimkakati, mahitaji ya dunia leo ni tani milioni 10, kufikia mwaka 2050 mahitaji yatakuwa tani tani laki 1 na nusu, sisi Tanzania tunabahati na kuwa nayo, tunaenda kuyapa kipaumbele ili utajiri huu tunufaike nao" amesema Mavunde.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa amewasihi Wachimbaji, Wafanyabiashara na watu wote wanaojihusisha na mnyororo mzima wa Sekta ya Madini kufuata utaratibu kwa kulipa kodi sambamba na kuepuka utoroshaji Madini ili Sekta ilifikie lengo lake kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa.
Uploading: 1064375 of 1940027 bytes uploaded.


Naye, Rais FEMATA John Bina, amesema kuwa Mchango wa Wachimbaji Wadogo umefikia asilimia 40 katika Sekta ya Madini kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya Madini kwa mwaka wa 2022/2023 ilinganishwa na mchango wa asilimia 8 tu ya mwaka 2016/2017.

Ameiomba serikali kupunguza kodi katika mitambo inayoingizwa hapa nchini kwa ajili ya kurahisisha uchimbaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi.

Aidha, Bina ameongeza kuwa FEMATA kwa kushirikiana na STAMICO wako kwenye hatua za mwisho za mchakato wa kuanzisha benki kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo nchini.
Uploading: 131000 of 2226808 bytes uploaded.


Nao baadhi ya wachimbaji wa madini waliohudhuria kikao hicho wameipongeza serikali kwa mikakati waliokuja nayo ili kukuza sekta ya madini pamoja na kubainisha kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni suala la mitaji.
Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)