ASKARI POLISI 4499 WAPANDISHWA VYEO SHULE YA POLISI MOSHI KILIMANJARO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Septemba 6, 2023 Askari Polisi 4499 wamepandishwa vyeo vya uongozi mdogo cheo cha Sagini meja (SM) na coplo (CPL) baada ya kufuzu mafunzo ya miezi mitatu kutoka vyeo vya awali Sagni (SGT) na Polisi Kontebo (PC) katika shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amewapongeza wahitimu hao kwa kufuzu na kupandishwa vyeo na umahiri mkubwa walioonyesha katika gwaride na maonyesho ya mbinu za medani.

Mhe. Sagini amewataka wahitimu hao kwenda kufanya kazi kwa weledi na kusimamia haki, kusimamia chaguzi zijazo kwa weledi mkubwa. “mmemaliza kipindi kizuri na nimejionea ukakamavu wenu na umahiri mkubwa mlionao, ni imani yangu na watanzania kuwa mtakwenda kutenda haki na kuimarisha ulinzi kwenye himaya zenu bila kuonea mtu” alisema Sagini.

Katika hatua nyingine Mhe. Sagini amempongeza Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha vyombo vya Usalama kufanya mafunzo mbalimbali na kuwapandisha vyeo. Aidha amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa kulisimamia Jeshi hilo na kuhakikisha Askari wanapata stahiki zao.

Pamoja na pongezi hizo Mhe. Sagini amelishauri Jeshi la Polisi kuwa na utaratibu wa kurudia mitihani kwa wahitimu wanaofeli mitihani ya mwisho ambayo inapelekea kukosa cheo. “Wahitimu hawa wameacha familia zao kwa ajili ya kutafuta cheo, anapomaliza leo na ukamwambia amefeli unamvunja moyo, nawashauri mkatazame upya utaratibu huu ikiwezekana kuwe na utaratibu wa kurudia mitihani kama utaratibu wa Nacte” alisema.

Aidha, Naibu Kamishna wa Polisi Mary Nzuki ambaye alimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura ambaye yuko kwenye majukumu mengine, amewataka wahitimu hao kuhakikisha wanatumia elimu na utaalamu walioupata katika kutanzua uhalifu katika maeneo yao. “yapo matukio mengi yanayogusa jamii hasa ya ukatili wa kijinsia yameshika kasi kwenye maeneo yenu, kahakikisheni uhalifu huu mnaumaliza kwa kutumia elimu na maarifa mliyoyapata kwenye mafunzo haya” alisema Nzuki.







Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)