TAMISEMI QUEENS YAPONGEZWA KWA KUENDELEA KUTETEA UBINGWA WA NETIBOLI 2023.

MUUNGANO   MEDIA
0

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Afya), Dkt. Wilson Mahera ameipongeza timu ya mpira wa Netiboli ya TAMISEMI QUEENS kwa kutwaa Ubingwa katika Ligi daraja la kwanza Netiboli mara mbili mfululizo.


Dkt. Mahera ametoa Pongezi hizo leo tarehe 30 Juni 2023 wakati akipokea Timu na Kombe cha Ushindi mara baada ya tumu kuwasili kTAMISEMI, jijini Dodoma wakitokea Dar es salaam kwenye mashindano.


Wakati akipongeza timu hiyo, Dkt. Mahera ameutaka Uongozi wa timu hiyo kuweka mpango mkakati wa kutumia timu hiyo kuendelea kutangaza kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.


Aidha, Dkt. Mahera amesema Ushiriki wa timu hiyo umekuwa na manufaa makubwa ambapo wachezaji sita wamechaguliwa kujiunga na timu ya Taifa ya netiboli

Amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kuunga mkono timu hiyo na kuiwezesha kuendelea kutwaa ubigwa katika Ligi mbalimbali na katika mashindano yatakayofanyika ndani na nje ya nchi.


Wakati huo, Dkt. Mahera amekabidhi zawadi kwa Wachezaji wote na Uongozi wa Timu hiyo, ikiwa ni pamoja na zawadi wa Mchezaji bora na mfugaji bora.







Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)