PROF. MAKUBI AKABIDHIWA OFISI RASMI NA KUANZA MAJUKUMU MOI
Author -
MUUNGANO MEDIA
Jumanne, Juni 13, 2023
0
Na Mwandishi wetu- MOI
Mkurugenzi
mtendaji mpya wa Taasisi ya tiba ya mifupa Muhimbili (MOI) Prof. Abel
N. Makubi amekabiziwa ofisi na mkurugenzi mtendaji aliyemaliza muda wake
Dkt. Respicious Boniface na kuanza majukumu yake rasmi.
Akizungumza
wakati wa makabiziano Prof. Makubi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa
nafasi ya kuisimamia Taasisi muhimu ya MOI ili kuendelea kuboresha
huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa
wananchi.
“Kwa namna ya pekee nimshukuru sana Waziri wa Afya Mh
Ummy Mwalimu (MB) Naibu Waziri, Katibu mkuu Wizara ya Afya, Mganga mkuu
wa Serikali pamoja na viongozi wengine wa Wizara kwa kuendelea
kuisimamia vyema sekta ya afya hapa nchini” Alisema Prof. Makubi.
Kwa
upande mwingine, Prof. Makubi ameomba ushirikiano wa dhati kwa
menejimenti na watumishi wote wa MOI ili kuhakikisha azma ya Serikali ya
awamu ya sita ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya
inatekelezwa.
“Wana MOI nimekuja kuwa mtumishi wenu, nimekuja
kuonyesha njia kwa kile Mh. Rais anachokitaka, anachokitaka Mh. Waziri,
mnachokitaka nyie pamoja na wanachokitaka wananchi” Alisema Prof.
Makubi.
Aidha, Prof. Makubi amepongeza mafanikio makubwa ambayo
Taasisi ya MOI imeyapata toka kuanzishwa kwake mwaka 1996. Pia
amepongeza bodi za wadhamini pamoja na wakurugenzi watendaji wote ambao
wameshawahi kuitumikia taasisi ya MOI ambapo amesema anathamini na
kutambua kazi zao za nyuma.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
wa MOI anayemaliza muda wake Dkt. Respicious Boniface amemshukuru Mh
Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan, Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu (Mb)
pamoja na viongozi wengine wa Wizara na Serikali kwa kupata nafasi ya
kuhudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 6. “Pia nitoe
shukrani za dhati kwa viongozi na watumishi wote wa MOI kwa ushirikiano
mlionipa katika kipindi chote naomba ushirikiano huo muendelee kumpa
Prof. Makubi kwa manufaa ya Taasisi yetu ya MOI na watanzania wote”
Alisema Dkt. Boniface