JAMII YATAKIWA KUWAFICHUA WANAO WAAJIRI NA KUWATMIKISHA WATOTO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na. Gideon Gregory, Dodoma.

Jamii imetakiwa kuendelee kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu wote wanaowaajiri na kuwatumikisha watoto.


Kauli hiyo imetolewa leo Juni 12,2023 na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mohamed Khamis Hamad wakati akiwasilisha tamko la tume hiyo mbele ya waandishi wa habari ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ajira kwa Watoto ulimwengini huku kauli mbiu ikiwa ni “Haki ya Jamii kwa Wote Kukomesha Ajira ya Watoto!”.


Amesema Kupitia kauli mbiu ya mwaka huu, THBUB inaendelea kuhamasisha jamii kuheshimu haki za binadamu katika masuala ya kazi na ajira.


“Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Sheria, Sera na Miongozo mbalimbali inayolinda haki za mtoto nchini,”amesema.


Pia amesema THBUB inatoa wito kwa Serikali, wadau na jamii kuunganisha nguvu kupinga ajira kwa watoto mahali popote nchini. 

Amesema pamoja na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa, bado zipo changamoto kadhaa, ikiwemo watoto kuendelea kufanyishwa kazi ngumu katika maeneo ya kazi za ndani, mashambani, mitaani, na migodini. 


“Ajira hizi zimekuwa kichocheo cha ukatili dhidi ya watoto ambapo baadhi yao hukosa masomo, kunyonywa kiuchumi kwa kuwa hulipwa ujira mdogo na matatizo ya kiafya, jambo linaloathiri ukuaji wao”,amesema.


Aidha, Hamad ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawatunza, kuwalinda na kuwapatia watoto mahitaji yao ya msingi pamoja na kuhudhuria shule na hawawatumii kama vitega uchumi vya familia kwa kuwafanyisha kazi ngumu, zisizofaa na zinazowaathiri. 

Kila ifikapo Juni 12 ya kila mwaka huadhimishwa siku ya Kimataifa ya Kupinga Utumikishwaji wa Mtoto Duniani – World Day against Child Labour ambapo siku hii ilizinduliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mwaka 2002 kama njia ya kuonyesha madhila wanayokutana nayo watoto wanaohusishwa katika ajira. 


 Shirika la Kazi kupitia Mkataba wa Kimataifa Na. 138, liliweka umri wa ajira kuwa miaka 15 na kuendelea na katika Mkataba Na. 182 liliorodhesha ajira zisizokubalika kwa watoto na ambazo zinatakiwa kuzuiwa. 

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)